Naomy Chesengeny – Swahili

Nairobi, Mji mkuu wa Safari duniani

Nililelewa vijijini nchini Kenya na kwa hivyo nilikua najua Nairobi tu kupitia picha kwenye kitabu changu cha masomo ya kijamii. Zilikuwa picha nzuri za majengo marefu, mabasi ya rangi mbalimbali, wanyamapori katika mbuga ya wanyama ya Nairobi, na picha za vituo vya kitamaduni kama vile Bomas of Kenya na African Heritage House iliyoko ndani ya jiji la Nairobi.Ninapenda kwenda mtandaoni kutafuta picha za Nairobi na picha iliyo hapa chini ilinivutia sana.

Paras Chandria

Nairobi ndio jiji pekee duniani lenye mbuga yake ya kitaifa. Hii ina maana kwamba ni mahali pekee duniani ambapo unaweza kupiga picha kama hii–picha ya twiga/wanyamapori mbele na majengo marefu yanayounda katikati mwa jiji.

Paras Chandria

Nilihamia Nairobi 2019 na nilipata uzoefu na kupenda jiji hilo kwa mara ya pili. Kuna maeneo mengi mazuri ya kutembelea kama vile maeneo ya vivutio vya utalii,migahawa, vituo vya ununuzi, na vituo vya burudani. Pia ni rahisi sana kuzunguka. Mabasi madogo – ambayo kwa kawaida hujulikana kama matatu – ni maarufu sana miongoni mwa wenyeji na watalii na mara chache hugharimu zaidi ya dola moja kusafiri popote ndani ya jiji.

Katika ukurasa huu wa tovuti, nataka kuzungumza kuhusu baadhi ya sehemu nzuri za kutembelea Nairobi kama mtalii na kwa nini nadhani unapaswa kuongeza jiji hili nzuri kama kivutio chako cha kitalii.

1. Hifadhi ya Taifa ya Nairobi

Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, ambayo iko maili sita tu kutoka katikati mwa jiji, ni nyumbani kwa wanyama wanne wa Big Five: vifaru, simba, chui na Duma. Neno, Big Five, linarejelea simba, chui, kifaru mweusi, tembo wa msituni wa Kiafrika, na duma wa Kiafrika na hapo awali lilibuniwa na wawindaji wa wanyamapori kurejelea wanyama wagumu zaidi barani Afrika kuwinda kwa miguu. Neno hili tangu wakati huo limekuwa maarufu miongoni mwa watalii na wenyeji na mara nyingi hutumika inaporejelea wanyama hawa watano kwa pamoja.

pexels
pexels

Mbuga hii inajulikana kuwa na msongamano mkubwa zaidi wa vifaru weusi nchini.

Wanyama wengine katika mbuga hii ni pamoja na twiga,pundamilia na fisi.

pexels

Hifadhi ya Nairobi pia ina kambi za mahema na hutumika na watalii wanaotafuta kutoroka msongamano wa jiji. Unapotembelea hifadhi hii, hutapata tu nafasi ya kwenda kupiga kambi lakini pia utaweza kujiandikisha kwa matembezi ya Safari. Hifadhi hii ina njia ya mbao iliyoinuliwa inayotumika kwa matembezi na inapitia mifumo yake mikuu mitatu ya ikolojia (Ardhi oevu, Savanna na Misitu). Vivutio vingine katika hifadhi hii ni pamoja na kituo cha wanyama yatima na jumba la makumbusho.

Hakikisha umeangalia tovuti ya hifadhi kwa maelezo zaidi kama vile maelekezo na ada za kuingia katika hifadhi

2.Giraffe Manor

Giraffe Manor ni hoteli ya kipekee ya boutique ambayo ni nyumbani kwa twiga wa Rothschild ambao hupenda kutembea karibu na nyumba ya manor

Picture from Giraffe Manor’s instagram

Baadhi ya shughuli utakazofanya wakati wa kutembelea manor ni pamoja na:

1.Kula kifungua kinywa na Twiga.

Picture from Giraffe Manor’s instagram

2.Kutembea kwa miguu kwenye Kituo cha Twiga

Picture from Giraffe Manor’s instagram
Picture from Giraffe Manor’s instagram

3.Kutembelea tembo yatima katika Shirika la Sheldrick Wildlife Trust

Picture from Giraffe Manor’s instagram

Vyanzo:

Big five:https://en.wikipedia.org/wiki/Big_five_game

https://www.kws.go.ke/parks/nairobi-national-park

Reflection:

Nilifurahiya sana kuandika blogi hii. Niliamua kuiandika kwa Kiingereza na kisha kuitafsiri kwa Kiswahili. Nina ufahamu sawa katika lugha zote mbili kwa hivyo kutafsiri haikuwa ngumu sana.Kutafsiri kutoka Kiingereza hadi Kiswahili bila shaka kulinifurahisha zaidi kwa sababu sipati kuandika kwa Kiswahili sana nje ya darasa hili.